Malkia Cixi wa China (29 Novemba 1835 – 15 Novemba 1908) alikuwa mwanamke Mchina aliyeshika utawala wa China kwa miaka mingi wakati wa karne ya 19 na mwanzoni mwa karne ya 20. Cheo chake rasmi ilikuwa "mjane wa kaisari" (mjane wa kifalme) akatawala kwa kushika mamlaka kwa niaba ya Kaisari wa nasaba ya Qing aliyekuwa mdogo mno. Katika mapokeo ya China ya Kale mama wa mtoto wa kifalme aliyerithi cheo cha baba alitawala kwa niaba ya mtoto kwa muda baada ya kifo cha Kaisari kama mtoto alikuwa bado mdogo.